Home Yanga SC MAJEMBE MANNE YA KAZI LEO KUTUMIKA NDANI YA YANGA KUIMALIZA MTIBWA SUGAR

MAJEMBE MANNE YA KAZI LEO KUTUMIKA NDANI YA YANGA KUIMALIZA MTIBWA SUGAR


 INGIZO jipya la Yanga, Fiston Abdoul Razack leo, Februari 20 linaweza kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mbali na Abdoul kuanza pia nyota Tonombe Mukoko naye huenda akaanza moja kwa moja kikosi cha kwanza baada ya mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar kwenye sare ya kufungana mabao 3-3 kuanzia benchi.

Hivyo leo Kocha Mkuu, Cedric Kaze ataanza na viungo wake wote wawili ambao ni washkaji wakubwa kutoka Congo, Tuisila Kisinda na Mukoko.

Kuhusu Abdoul inaelezwa kuwa aliomba kukaa kando kwa kuwa alikuwa kwenye presha kubwa mara baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City pamoja na ule wa kirafiki dhidi ya African Lyon.

Kaze aliweka wazi kwamba sababu ya Tonombe kuanzia benchi kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera ni kumpumzisha kwa kuwa wana mechi nyingi hivyo atamtumia kwenye mechi zake zijazo.

“Tonombe alikuwa benchi kwa kusudio maalumu hasa ukizingatia kwamba tuna mechi nyingi za kucheza hivyo ilikuwa ni lazima nipumzishe wachezaji,” alisema.

Habari zinaeleza kuwa huenda leo Yacouba Songne ambaye anasumbuliwa na majeraha pamoja Saido Ntibanzokiza watacheza pia kwa kuwa wanahitaji ushindi.

“Ujue Ntibanzokiza alicheza mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi akiwa na majeraha ya nyonga hivyo anaweza kuanza pia mbele ya Mtibwa Sugar, hata Yacouba inawezekana maana kwa sasa timu inahitaji ushindi,” ilieleza taarifa hiyo.

SOMA NA HII  KUHUSU KIWANGO CHAKE KUSHUKA...FEI TOTO AVUNJA UKIMYA YANGA...AMNYOOSHEA KIDOLE NABI...