Home Habari za michezo BAADA YA KUUONA MZIKI WA MAMELOD DAR….AZIZ KI KAFUNGA MACHO KISHA AKASEMA...

BAADA YA KUUONA MZIKI WA MAMELOD DAR….AZIZ KI KAFUNGA MACHO KISHA AKASEMA HILI KUBWA…

Habari za Yanga leo

Kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki amesema kwenye mchezo wa kwanza hatua ya robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowans walitumia akili nyingi na nguvu, licha ya kukosa umiliki mkubwa wa mchezo.

Pia amesema kuelekea mchezo wa Ijumaa ugenini bado mbinu ndizo zitakazoamua matokeo, huku akikiri kuwa wataendelea kuwapa heshima Mamelodi wakipanga kupata matokeo katika dakika za mwanzo cha mchezo.

Yanga ilikutana na Mamelodi Jumamosi wiki iliyopita na Ijumaa watashuka dimbani tena ugenini tayari kwa ajili ya kusaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Aziz Ki amesema mbinu nzuri za benchi la ufundi chini ya kocha Miguel Gamondi na wao kama wachezaji, zilifanya kazi kwa dakika 180 sio 90 kama wengi wanavyozungumza kutokana na namna walivyojituma na kupambana.

“Mchezo uliopita kwangu ni kama tulitumia dakika 180 kwani ulikuwa mgumu na wenye mbinu kali ambazo kwa asilimia 80 zililipa kwani 20 ni namna ambavyo tulishindwa kupata bao licha ya kutengeneza nafasi,” amesema.

“(Watu) wamekuwa wakizungumza kuwa tulikuwa uwanja wa nyumbani, lakini hatukuwa na malengo ya kufunga. Sio kweli mbinu yetu licha ya kutomiliki mpira tulifanikiwa kwani hata aliyemiliki hakuwa na nafasi ya kutengeneza mashambulizi.”

Aziz Ki amesema mchezo uliopita umewapa mpango wa namna gani watafanya ili kuweza kujihakikishia nafasi ya hatua ya nusu fainali ugenini, huku akiweka wazi kuwa wana imani kubwa ya kufanya vizuri kwani matokeo ya nyumbani yanawapa nguvu.

“Kutopata matokeo nyumbani na kuto kuruhusu bao ni mpango mzuri ambao unatupa imani kuwa tukitumia vyema nafasi ugenini tutakuwa na uhakika wa kuvuka hatua i ayofuata hasa kwa kupata matokeo dakika za mapema,” amesema.

“Pia ugumu upo kwani mpinzani naye atajipanga kuhakikisha uwanja wake wa nyumbani hafanyi makosa kama nasi tulivyofanya hivyo mbinu bado zitaendelea kuamua nani atinge hatua inayofuata.”

Aziz Ki amesema licha ya mbinu za kocha Gamondi wao pia kama wachezaji watafanya kila linalowezekana ili kuweza kuhakikisha wanafikia lengo la kutinga hatua inayofuata.

SOMA NA HII  BOCCO AKABIDHIWA MIL 35...NI ILE AHADI YA MAMA SIMBA...IKISHINDA DHIDI YA HOROYA