Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI vs AL AHLY…KAGERE KAWEKA ‘UNAFKI’ PEMBENI….KAWAPA UKWELI HUU SIMBA…

KUELEKEA MECHI vs AL AHLY…KAGERE KAWEKA ‘UNAFKI’ PEMBENI….KAWAPA UKWELI HUU SIMBA…

Habari za Michezo leo

STRAIKA wa Namungo FC, Meddie Kagere anaamini Simba ina nafasi ya kushinda mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Alhy, akiwataka wachezaji kutokata tamaa na kuona wanakwenda kukamilisha ratiba.

Mwaka 2019 Kagere akiwa Simba aliyeifungia bao ilipoibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Alhy katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, amesema ndani ya dakika 90 lolote linaweza kutokea, hivyo anaamini mchezo wa Ijumaa utakaopigwa saa 5:00 usiku upo wazi.

“Simba ina uzoefu mkubwa kimataifa. Ina kikosi kizuri kinachoweza kubadili mitazamo ya watu kuona mwisho wa mchezo wao ulikuwa nyumbani,” alisema.

“ Ahly na wao wenyewe wana presha kama inavyokuwa kwa Simba, jambo ambalo nani anashinda litatakiwa kuamuliwa na dakika 90. Nawaamini watafanya maajabu na wanaweza wakaishangaza.”€ Kagere aliondoka Simba akiwa amenyakua mataji matatu ya Ligi Kuu na kufunga mabao 65 katika misimu ya 2018/19, 2019/20 na 2020/21.

SOMA NA HII  STRAIKA WA POLISI TZ ALIYEVUNJIKA MIGUU YOTE AMLILIA MAMA SAMIA KWA UCHUNGU