Home Uncategorized NAMUNGO FC: HAIKUWA RAHISI KUSHINDA MBELE YA MBEYA CITY

NAMUNGO FC: HAIKUWA RAHISI KUSHINDA MBELE YA MBEYA CITY


 OFISA Habari wa Namungo FC ,Kidamba Namlia amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Mbeya City ulikuwa mgumu licha ya kushinda kwa bao 1-0 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Bao pekee la ushindi lilipachikwa kimiani na Bigirimama Blaise dakika ya 10 akiwa ndani ya 18 na kuwafanya Mbeya City kuyeyusha pointi 12 kwenye mechi zake nne kwa msimu wa 2020/21.

Akizungumza na Saleh Jembe, Namlia amesema kuwa wachezaji waliambiwa kwamba wanacheza na timu ngumu ambayo imepoteza mechi zake zote ndani ya ligi.

“Ilikuwa ngumu kushinda mbele ya Mbeya City na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery aliwaambia wachezaji kwamba utakuwa mchezo mgumu. Kilichotokea ni kwamba tulikuwa tunahitaji kupata ushindi na hicho ndicho ambacho kimetokea,” amesema.

Namungo inarejea Lindi ambapo itakuwa na mchezo dhidi ya Mwadui FC pamoja na Kagera Sugar Uwanja wa Majaliwa.

Namungo imeambulia pointi tatu baada ya kutoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons na Mbeya City ilitoka kupoteza mbele ya Azam FC kwa kufungwa bao 1-0.

SOMA NA HII  DITRAM NCHIMBI: NINAFANYA MAZOEZI KULINDA KIWANGO CHANGU