Home Uncategorized MTIBWA SUGAR:TUNABOMOA NGOME YA YANGA

MTIBWA SUGAR:TUNABOMOA NGOME YA YANGA

 


UONGOZI wa Mtibwa Sugar, umesema kuwa haitakuwa kazi rahisi kwa wapinzani wao Yanga kupenya kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri.


Mchezo huo ni wa raundi ya nne ambapo utawakutanisha Mtibwa Sugar na Yanga zote zikiwa zimetoka kushinda mechi zao za hivi karibuni kwa msimu wa 2020/21.


Yanga wenyewe wametoka kushinda kwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar huku Mtibwa Sugar ikishinda bao 1-0 mbele ya Ihefu FC.


Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wamejipanga vilivyo kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga.

“Haitakuwa nafasi ya wapinzani wetu Yanga kutushinda siku ya Jumapili, tutabomoa ngome yao kuhakikisha kwamba tunashinda mechi yetu tunabomoa tu, tutapiga Yanga siyo Yanga wanajiita Wananchi.


“Tuna kikosi kizuri tofauti na msimu uliopita ambapo mambo yalikuwa magumu kwetu ila kwa sasa tupo tofauti, tuna washambuliaji wazuri ambao wana nguvu na uchu wa kufunga tumewatoa Zanzibar, wapo tayari kupambana hivyo ni suala la kusubiri,” amesema ,” hobias Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar

SOMA NA HII  MEDDIE KAGERE: NINAIPENDA KAZI YANGU