Home Uncategorized KMC YAPOTEZA KWA KUFUNGWA BAO 1-0 MBELE YA KAGERA SUGAR

KMC YAPOTEZA KWA KUFUNGWA BAO 1-0 MBELE YA KAGERA SUGAR


 MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Yusuph Mhilu leo Septemba 25 ikiwa ni mechi yake ya kwanza kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara  dhidi ya KMC amefunga bao moja na kuipa timu yake pointi tatu mazima.
Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya wababe KMC ambao walikuwa wamecheza mechi tatu mfululizo bila kupoteza ndani ya ligi kwa msimu huu na walifunga jumla ya mabao nane na kibindoni kujiwekea pointi tisa.


Huu ni mchezo wa kwanza kwa Kagera Sugar kushinda Uwanja wa Kaitaba na ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa ilicheza mechi tatu bila kushinda, ilipoteza mbili na kuambulia sare moja.

Ilianza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania Uwanja wa Kaitaba na kulazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Gwambina FC Uwanja wa Gwambina Complex kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga, Kaitaba.

Msimu wa 2019/20 Mhilu alipachika jumla ya mabao 13 na kuwa miongoni mwa wazawa wenye ushkaji na nyavu.

Kagera Sugar inafikisha jumla ya pointi nne na kuwa nafasi ya 13 na KMC inabaki nafasi ya kwanza ikiwa na pointi tisa.
SOMA NA HII  AZAM FC: MAPAMBANO BADO YANAENDELEA, AKILI ZETU SASA NAMUNGO