Home Yanga SC YACOUBA, JEMBE LA KAZI NDANI YA YANGA KUIBUKIA MKWAKWANI

YACOUBA, JEMBE LA KAZI NDANI YA YANGA KUIBUKIA MKWAKWANI


 MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Yanga, Yacouba Songne huenda kesho ataanza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ya Tanga baada ya kukosekana uwanjani kwa muda.

Nyota huyo raia wa Burkina Faso alikuwa nje ya uwanja akitibu maumivu yake ya mgongo ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

Hakuwa kwenye kikosi kilicholazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar wala kile kilichoshinda ba 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa.

Pia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora hakuwa sehemu ya kikosi hicho wakati Yanga ikishinda bao 1-0.

Yupo na kikosi ambacho kipo Tanga kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union ambapo alikuwa kwenye sehemu ya kikosi cha kwanza  kilichoshinda mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa.

Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na kufunga mabao 34 amehusika kwenye mabao nane ambapo amefunga mabao manne na ametoa jumla ya pasi nne za mabao.


Alifungua akaunti yake ya mabao mbele ya Coastal Union ya Juma Mgunda kwa pasi ya mshkaji wake Mukoko Tonombe.


Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa kurejea kwa nyota huyo ndani ya uwanja ni nguvu ya kikosi kuendelea kusaka ushindi.

“Yacouba naye hali yake ni njema hivyo kurejea kwake ndani ya uwanja kunaongeza upana wa kikosi na hilo ni jambo jema kwa timu,”.
SOMA NA HII  GAMONDI KUWABADILISHAI 'GIA ANGANI' AL AHLY.....MPANGO MPYA WASUKWA KIMYA KIMYA...