Home news NYOTA MTIBWA SUGAR AJIFUNGA POLISI TANZANIA

NYOTA MTIBWA SUGAR AJIFUNGA POLISI TANZANIA


 MSHAMBULIAJI wa Mtibwa Sugar, Mohamed Hilika msimu ujao atakuwa na jezi ya Polisi Tanzania baada ya kusaini dili jipya katika timu hiyo.

Nyota huyo alikuwa kwenye ubora wake kwenye mechi ya mwisho ya mchezo wa mtoano ambapo aliweza kufunga mabao matatu na kusepa na mpira wake.

Ilikuwa mbele ya Transit Camp, Uwanja wa Uhuru, Julai 21 na alitupia mabao hayo dakika ya 9,70 na 84.

Mshambuliaji huyo amesema:”Nimejiunga na Polisi Tanzania ninafurahi kufanya hivyo. Nimekuja kupata changamoto mpya na nitajitahidi kufanya vizuri,”.

Chanzo:Championi 

SOMA NA HII  MCHAMBUZI: YANGA WAHAJAFANIKIWA KIMATAIFA....LABDA SIMBA KWA KUWA WANA NGAO ...