Home kimataifa RONALDO AANZA MPANGO WA KUTAFUTA TIMU KWA SASA

RONALDO AANZA MPANGO WA KUTAFUTA TIMU KWA SASA


 INAELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Juventus, Cristiano Ronaldo dili lake la kurejea Real Madrid kubuma ameanza kutafuta timu nyingine.

Hivi karibuni habari zilieleza kwamba Ronaldo yupo kwenye hesabu za kurudi Madrid ila timu yake hiyo ya zamani iliamua kumpotezea kwa kueleza kuwa haina mpango naye kwa sasa.

Mkataba wake ndani ya Juventus umesalia muda wa mwaka mmoja na mengi waliyotarajia mabosi wake kupata kutoka kwake yameshindikana jambo ambalo linaonyesha kwamba hataongezewa mkataba.

Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya imeshindwa kufanya vizuri baada ya kutolewa na hawana nafasi ya kutwaa ubingwa wa Serie A jambo ambalo linaongeza ugumu kwa staa huyo kubaki katika timu hiyo.

Wakala wa mchezaji huyo, Jorge Mendes alishakutana na bodi ya Manchester United na inaonekana itakuwa ngumu kurudi, pia timu nyingine inayotajwa ni PSG nayo inawania saini ya nyota huyo.

SOMA NA HII  SAFARI YA NOVATUS ULAYA HAIKUWA KINYONGE....