Home Uncategorized WATATU WATAJWA KURITHI MIKOBA YA SVEN SIMBA, MMOJA YUPO BONGO

WATATU WATAJWA KURITHI MIKOBA YA SVEN SIMBA, MMOJA YUPO BONGO


IMEELEZWA kuwa kwa sasa kuna majina matatu ambayo yanatajwa kuingia kwenye orodha ya wale ambao wanatafutwa kurithi mikoba ya Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji.

Kocha wa zamani wa Al Ahly, Rene Weiler aliyepata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri, Kombe la FA la Misri kabla ya kutimuliwa hivi karibuni kumpisha Pitso Mosimane kutoka Afrika Kusini anatajwa kuwa kwenye rada za Simba.

Pia Florent Ibenge anayeinoa timu ya taifa ya DR Congo na AS Vita yupo kwenye rada za Simba.


Ibenge kwa sasa yupo Bongo akiwa na timu ya Taifa ya Congo ambayo leo inacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Pia Kocha Msaidizi wa Raja Casablanca, Hicham Aboucherouane naye anatajwa kuwa miongoni mwa makocha ambao wameomba kazi ndani ya kikosi hicho ambacho kesho kitacheza mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa mchakato upo sawa na wana amini kwamba watampata mtu sahihi ndani ya kikosi hicho.


SOMA NA HII  AJIBU KUTOKUWEPO NDANI YA SIMBA MSIMU UJAO