Home Uncategorized SIMBA:TUTAWAFURAHISHA MASHABIKI MBELE YA YANGA

SIMBA:TUTAWAFURAHISHA MASHABIKI MBELE YA YANGA


 MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Klabu ya Simba amesema kuwa watawafurahisha mashabiki wao kesho kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.

Yanga inakutana na Simba baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Azam FC baada ya dakika dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Inakutana na Simba ambayo imetinga hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo FC.

Simba kweye mechi tatu imetupia jumla ya mabao 7 ambapo Yanga kwenye mechi tatu imetupia mabao mawili ndani ya dakika 90.

Kagere ametupia mabao mawili na kinara wa utupiaji ni Miraj Athuman mwenye mabao manne ndani ya Klabu ya Simba.

Mshambuliaji huyo amesema:”Tukiwa uwanjani tunafikiria kupata matokeo kwa ajili yetu na mashabiki ili kuona namna gani tunafikia malengo yale ambayo tumejiwekea.

“Kuelekea kwenye mchezo wetu wa fainali nina amini kwamba tutawafurahisha mashabiki wetu watakaojitokeza uwanjani na wale ambao watashindwa kufika uwanjani,” .

SOMA NA HII  RUVU YAPIGA PANGA WATANO