Home Habari za michezo KISA KIWANGO CHA OKRAH…SIMBA WAKOSA MAMILIONI KUTOKA FIFA…WANGELAMBA BINGO NONO…

KISA KIWANGO CHA OKRAH…SIMBA WAKOSA MAMILIONI KUTOKA FIFA…WANGELAMBA BINGO NONO…

Habari za Simba

Matumaini ya Simba kupata zaidi ya Sh206 milioni kutoka Shrikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) yameyeyuka rasmi baada ya nyota wake Augustine Okrah kutoteuliwa kuwemo katika kikosi cha Ghana kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar baadaye mwezi huu hadi Disemba mwaka huu.

Kiasi hicho cha fedha ambacho Simba ingevuna ni kile ambacho Fifa inatoa kwa kila klabu ambayo mchezaji wake anashiriki katika fainali hizo kwa kila siku ambayo timu yake itakuwepo kuanzia katika mechi za hatua ya makundi hadi hatua ambayo itaishia.

Kwa mujibu wa utaratibu, Fifa hutoa kiasi cha Dola 10,000 (Sh22.9 milioni) kulipa klabu kwa kila siku ambayo mchezaji wake mmoja amekuwa akiwakilisha nchi yake katika mashindano hayo na iwapo Okrah angekuwepo katika kikosicha Ghana, kwa siku tisa tu ambazo timu yake ya taifa ingezitumia kucheza mechi tatu za hatua ya makundi, Simba ingeweza kuvuna kiasi cha Dola 90,000 (Sh206 milioni).

Ghana itacheza mechi ya kwanza ya kundi H la mashindano hayo kwa kuvaana na Ureno kisha mechi ya pili watacheza dhidi ya Korea Kusini, Novemba 28 na mchezo wa mwisho watacheza Disemba 2 dhidi ya Uruguay.

Katika kikosi cha awali cha wachezaji 55 kilichotangazwa jana na kocha Otto Add, hakuna jina la Augustine Okrah ambaye aliwahi kuwemo katika kikosi kilichokuwa kikicheza mechi za kuwania kufuzu fainali hizo huku kikijaza kundi kubwa la nyota wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Kikosi cha Ghana kinaundwa na wachezaji Joseph Wollacott, Ibrahim Danlao, Abdul Manaf Nurudeen, Richard Ofori, Lawrence Ati Zigi, Denis Odoi, Tariq Lamptey, Alidu Seidu, Baba Abdulrahman, Gideon Mensah, Patrick Kpozo, Ibrahim Imoro, na Dennis Korsah.

Nyota wengine katika kikosihicho cha watu 55 ni Alexander Djiku, Mohammed Salisu, Abdul Mumin, Jonathan Mensah, Daniel Amartey, Joesph Aidoo, Stephan Ambrosius, Kasim Adams, Thomas Partey, Baba Idrissu, Mubarak Wakaso, Elisha Owusu, Mudasiru Salifu, Abdul Salis, Andre Ayew, Majeed Ashimeru, Joseph Paintsil, Mohammed Kudus, Daniel Kyereh, Daniel Afriyie na Jeffrey Schlupp.

Wapo pia Jordan Ayew, Kamaldeen Suleimana, Mohammed Dauda, Ernest Muamah, Yaw Yeboah, Emanuel Gyasi, Abdul Fatawu Issahaku, Osman Bukari, Ransford Yeboah, Kamal Sowah, Samuel Owusu, Christopher Antwi-Adjei na Joel Fameh.

Wengine ni Inaki Williams, Felix Gyan, Antoine Semenyo, Kwasi Wriedt, Caleb Ekuban na Richmond Boakye.

SOMA NA HII  DAH...CHAMA NDIO BASI TENA ....AFUNGUKA SHIDA ANAYOIPITIA SIMBA...HATACHEZA KWA MWEZI MZIMA...