Home Habari za michezo SIKU ZA KISINDA YANGA ZAHESABIKA…KAMBOLE AWEKWA TAYARI KUCHUKUA NAFASI…

SIKU ZA KISINDA YANGA ZAHESABIKA…KAMBOLE AWEKWA TAYARI KUCHUKUA NAFASI…

Yanga tayari ipo Tunisia baada ya kuondoka juzi mchana na kulala Dubai, huku makocha wa timu hiyo wakiwa na presha kubwa ya mechi ya marudiano ya ugenini dhidi ya Club Africain ya huko, lakini Za Ndaani Kabisa zinasema Yacouba Songne na Lazarious Kambole wanarudishwa kikosini.

Kambole na Songne wapo katika kikosi hicho wakilipwa kila kitu, licha ya kutotumika kutokana na kutosajiliwa msimu huu, lakini Za Ndaani Kabisa, zinasema mastaa hao watarejeshwa kikosini rasmi dirisha dogo, wakipishana na baadhi ya nyota waliochemsha kwa sasa watakaotemwa au kutolewa kwa mkiopo.

Nyota wanaoweza kutolewa kwa mkopo ni Joyce Lomalisa, Heritier Makambo, Tuisila Kisinda na Jesus Moloko ambao wamekuwa na viwango vya kawaida tofauti na walivyotarajiwa.

Kutokana na kanuni kwa klabu kuruhusiwa kusajili nyota wa kigeni 12, Yanga inajipanga kuwatoa kwa mkopo au kumalizana kabisa na mastaa hao ili kuwapisha Kambole ambaye alisajiliwa na kukumbwa na majeraha kabla ya kutangazwa kupelekewa Uganda ili kumpisha Kisinda na mwishowe kusalia Jangwani akihudumiwa kila kitu na kama ilivyo kwa Songne aliyekuwa majeruhi wa muda mrefu.

“Kwa namna wachezaji hao wawili wanavyojituma mazoezini, japo hawatumiki, mabosi wameona ni vyema wakaongezwa kwenye dirisha dogo kuchukua wale watakaotemwa au kutolewa kwa mkoko kutokana na kushindwa kuibeba timu kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa,” kilisema chanzo kutoka ndani ya klabu hiyo.

Inaelezwa kuchemsha kwa baadhi ya nyota waliotumainiwa kuibeba timu Ligi Kuu Bara na michuano ya CAF, imewatibua mabosi wa klabu hiyo na sasa wanapata shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wanaotaka wapigwe chini kwani hawana msaada.

SOMA NA HII  IMEFICHUKAAH....MSHAHARA WA KOCHA MPYA SIMBA NI KUFRU....KULIPWA ZAIDI YA MIL 50 KWA MWEZI...