Home Yanga SC HII HAPA ORODHA YA NYOTA NANE WENYE UHAKIKA WA KUBAKI YANGA

HII HAPA ORODHA YA NYOTA NANE WENYE UHAKIKA WA KUBAKI YANGA


IMEELEZWA kuwa nyota nane wa Yanga kwa sasa wana uhakika wa kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2021/22 huku wengine wakisubiri ripoti ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Miongoni mwa nyota ambao mpaka sasa hawajui hatma yao na wana asilimia kubwa ya kusepa ndani ya kikosi hicho ni pamoja na mshambuliaji Fiston Abdulazack ambaye mkataba wake msimu ukiisha naye mkataba wake unameguka.

Hana uhakika wa kubaki Yanga kwa kuwa hajaitwa kuzungumza na mabosi wake na kipengele cha kuongeza mkataba wake inaeleza kuwa kilikuwa kinaeleza kuwa itategemea na uwezo wake ambao atauonyesha ila mpaka sasa amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza.

Taarifa zimeeleza kuwa nyota ambao wana uhakika wa kubaki ndani ya Yanga kwa msimu ujao ni wale ambao walikuwa wanaanza kikosi cha kwanza katika mechi tatu zilizopita chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ni pamoja na:-Saido Ntibanzokiza, Yacouba Songne, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Kibwana Shomari, Dickson Job, Feisal Salum, Abdalah Shaibu, ‘Ninja’.

Kuhusu suala hilo, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa suala la usajili lipo mikononi mwa kocha.

“Jukumu la usajili ni la kocha, katika hilo kuelekea msimu ujao kila kitu tumemuachia yeye, hivyo ndiyo sababu ya kumuwahisha kuja kumaliza msimu kwa kuangalia wachezaji wengi,” alisema.

Chanzo: Spoti Xtra

SOMA NA HII  MAYELE ATUPA JIWE GIZANI BAADA YA AZAM KUPOKEA KIPIGO DHIDI YA YANGA