Home news KUELEKEA MECHI YA LEO..AHMED ALLY AFUNGUKA WALIYOYAGUNDUA..ATAJA WATAKAOKOSEKANA…

KUELEKEA MECHI YA LEO..AHMED ALLY AFUNGUKA WALIYOYAGUNDUA..ATAJA WATAKAOKOSEKANA…


SIMBA inafanya mazoezi yake ya mwisho jana saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Highland mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wao wa 12 dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa dimba la Manungu, Tuliani.

Afisa Habari wa timu hiyo, Ahmed Ally amesema nje ya Jonas Mkude na Kibu Denis ambao ni majeruhi, wengine wapo salama na morali ya urejesha kicheko kwa mashabiki wao.

Amesema anatambua utakuwa mchezo mgumu, lakini chini ya kocha wao Pablo Franco watafanya jambo la kutetea heshima ya klabu.

“Tunajua hakuna mechi rahisi, Mtibwa Sugar katika mechi zake 12 imeshinda mbili, sare tano na wamefungwa tano, sasa hawawezi kuzindukia kwetu,”amesema na ameongeza kuwa;

“Tunawaomba mashabiki wetu,tushikamane  kwa pamoja,kuhakikisha tunawapa moyo wachezaji wetu ambao wanatuwakilisha uwanjani ili kutimiza malengo yetu ya kutetea  ubingwa,” amesema.

Amesema  wanaichukulia kila mechi kama fainali, hivyo wamesahau matokeo yaliopita na wanaelekeza nguvu zao kwenye kupambania pointi ambazo zipo mbele yao.

“Kila mechi kwetu ni muhimu, kwani tunajua uwingi wa pointi ndio matokeo ya ubingwa,”amesema.

SOMA NA HII  BENCHIKAH KUREJEA TENA SIMBA...AFANYA KAZI SIKU 156 TU...ASHANGAZWA NA MASHABIKI