Home Habari za michezo HAWA HAPA MASTAA 5 WA SIMBA SC WALIOKALIA KUTI KAVU…TARAJIA LOLOTE…

HAWA HAPA MASTAA 5 WA SIMBA SC WALIOKALIA KUTI KAVU…TARAJIA LOLOTE…

Habari za Simba

Wakati mabosi wa Simba wakiwa kwenye harakati za kuboresha kikosi chao dirisha hili dogo la usajili kuna wachezaji watatu hadi sasa ni suala la muda tu kutua ndani ya timu hiyo.

Inaelezwa mabosi hao wa Simba kwenye kipindi cha usajili wamepanga kushusha mashine mpya si chini ya tano kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kwenye maeneo tofauti kulingana na mapungufu ya mzunguko wa kwanza.

Simba ina nafasi moja ya kusajili mchezaji wa kigeni hadi wakati huu iliyoachwa wazi na mshambuliaji raia wa Serbia Dejan Georgijevic aliyetimka ndani ya kikosi hicho mapema kwenye mzunguko wa kwanza.

Simba kama itafanikiwa kusajili zaidi ya mchezaji mmoja wa kigeni maana yake wageni waliyopo ndani ya kikosi kwa sasa kuna watakaonyeshwa mlango wa kutoka ili nafasi ipatikane za wapya kuingia.

Kuna nyota kama, Victor Akpan, Nelson Okwa wapo kwenye wakati mgumu na huenda wakaonyeshwa mlango wa kutokea kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara.

Wakati huo huko kuna timu tofauti kwenye Ligi Kuu Bara zinampango wa kutuma maombi ya kuwaomba wachezaji wa Simba kwa mkopo kama, Kibu Denis, Nassoro Kapama, Jimsony Mwanuke na wengineo.

Wachezaji hao huenda wakaombwa kwa mkopo kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho cha Simba katika michezo mfululizo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWAKOSA WAARABU...BOCCO ASHUSHA 'PRESHA' SIMBA..DAKTARI AFUNGUKA A-Z...