Home Habari za michezo KLABU HII BONGO YAFUNGIWA…MCHEZAJI ASHINDA KESI YA MADAI…TFF WAGEUKA MBOGO

KLABU HII BONGO YAFUNGIWA…MCHEZAJI ASHINDA KESI YA MADAI…TFF WAGEUKA MBOGO

Uwanja wa Mkapa

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Tabora United mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake, Jean Didie Touya baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Mchezaji huyo raia wa Cameroon alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba ambapo klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Taarifa ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imebainisha kuwa wakati FIFA ikiifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, TFF imeifungia Tabora United kufanya uhamisho wa ndani.

“TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.” imesema sehemu ya taarifa ya TFF.

SOMA NA HII  DODOMA JIJI HALI SI HALI....MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU...'WAFINYWA KISELA' NA NAMUNGO