Home news KISA KUKAZIWA NA MBEYA CITY…AUCHO NA MAYELE WAPEANA ‘MAKAVU LIVE’ MAZOEZINI…NABI AIBUKA...

KISA KUKAZIWA NA MBEYA CITY…AUCHO NA MAYELE WAPEANA ‘MAKAVU LIVE’ MAZOEZINI…NABI AIBUKA NA HILI JUU YAO…


YANGA iko katika ratiba ya mazoezi makali ya mara mbili kwa siku, lakini Kocha Nesredinne Nabi ameshtushwa na moto aliouona mazoezini.

Nabi alisema kwamba mastaa wote akiwemo Fiston Mayele, Khalid Aucho na wengine wameanzisha umoja wa aina yake mazoezini kwenye mambo mbalimbali tofauti na awali.

Kocha huyo anasema kwamba wamekuwa wakikosoana sana na kusaidiana pale mmoja anapokosea lakini mambo mengi wamekuwa wakipambana kwa nguvu za ziada huku chanzo kikionekana ni matokeo ya suluhu dhidi ya Mbeya City Jijini Dar es Salaam.

Anasema kwamba muitikio walioupata mastaa baada ya matokeo ya Mbeya City kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki, wanachama pamoja na uongozi umewashtua na kuwapa mzuka zaidi ya kuipambania klabu hiyo kuelekea ubingwa kwani wamejua hali halisi ya msimu huu.

“Nafurahi kuona kila mchezaji yuko makini sana katika programu ya mazoezi huku ni kitu kilichonishtua muamko wa namna hii kuna kitu unamaanisha,”alisema Nabi.

“Kujituma huku kwa wachezaji kutatupa wakati mzuri wa kurejea katika njia yetu ya ushindi hakuna ambaye alifurahia ile sare,hiki ndicho ninachokiona sasa na kila mmoja anataka kuona tunafuta hayo matokeo,”aliongeza Kocha huyo ambaye mashabiki wa Yanga wamempachika jina la Profesa.

Staa wa zamani wa Yanga, Abeid Mziba ‘Tekelo’ alisema Yanga watakuwa wameonyesha nidhamu hiyo ni hatua kwamba waliumia na suluhu.

Mziba ambaye alikuwa anafunga mabao makali ya vichwa alisema wachezaji wa Yanga walichofanya ni kuendelea na misingi ya klabu hiyo kama miaka ya nyuma.

“Unapopata suluhu nyumbani huku ukiwa unapata kila kitu lazima utaumia,hawakucheza vibaya Hiki walichofanya ndio msingi wa Yanga hata sisi tulikuwa tunahamasishana wenyewe tunapopata matokeo ya kutushtua kama yale kitu ambacho kocha na hata wao wachezaji wanatakiwa kukifanyia kazi ni kujiimarisha kushambulia wakitokea pembeni.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUSAFISHWA NA TFF...MGUNDA KAFUNGUKA HAYA SAKATA LA LESENI YAKE...