Home Uncategorized DAVI DE GEA ATAFUTIWA MBADALA WAKE

DAVI DE GEA ATAFUTIWA MBADALA WAKE


DAVID De Gea mlinda mlango wa Manchester United amekuwa kwenye wakati mgumu msimu huu kutokana na kufanya makosa mengi ya kiufundi jambo linalohatalisha nafasi yake ndani ya kikosi hicho ambapo inaelezwa kuwa uongozi wa United umeanza kufanya mazungumzo na Dean Henderson anayekipiga Kwa mkopo Sheffield ili arejee ndani ya kikosi hicho.

De Gea alijiunga na United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid na amekuwa akipewa nafasi ya kuanza kwenye mechi nyingi.

Ameanza kikosi cha Kwanza kwenye jumla ya mechi 393 mpaka sasa. Henderson mwenye miaka 22 anapewa nafasi kubwa kurejea.

Kosa lake la kiufundi alilofanya Jumapili wakati timu yake ililazimisha Sare ya bao 1-1 baada ya kufungwa na Dominic Calvert-Lewin limezua mjadala wengi wakiamini alimpa zawadi ya bao nyota huyo .

Ole Gunnar Solskjaer , Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa De Gea ni mlinda mlango bora duniani.

SOMA NA HII  TFF YASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU NA SERENGETI PREMIUM LAGER