Home Uncategorized KOCHA ARSENAL AWASIFU WACHEZAJI WAKE ASEMA HAWAJAMUANGUSHA

KOCHA ARSENAL AWASIFU WACHEZAJI WAKE ASEMA HAWAJAMUANGUSHA

ARSENAL imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la FA, England baada ya kushinda kwa mabao 2-0 mbele ya Portsmouth.

Mabao ya Arsenal iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta yalifungwa na Sokratis Papastathopoulos dakika ya 45+4 na lile la pili lilipachikwa na Eddie Nketiah dakika ya 51.

Arteta amesema kuwa wachezaji wake hawajamuangusha katika hilo anaamini watafanya vizuri hatua ya mbele.

“Wametumia nguvu nyingi katika kazi wamefanya kinachostahili naheshimu mchango wao na ninatambua kile walichokifanya, wanastahili na ninafurahi kufanya nao kazi,” amesema .

SOMA NA HII  MDAMU: TUPO TAYARI KUPAMBANA MBELE YA MBAO FC