Home Habari za michezo BAADA YA KUMUONA MAYELE ANAVYOTESEKA KUTETEMA…NABI KATIKISA KICHWA WEE…KISHA AKASEMA HAYA…

BAADA YA KUMUONA MAYELE ANAVYOTESEKA KUTETEMA…NABI KATIKISA KICHWA WEE…KISHA AKASEMA HAYA…


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga SC Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kilikosa bahati ya kufunga kwenye michezo mitatu ya Ligi Kuu iliyopita ambayo yote walitoka suluhu. Amesema hayo kuelekea mchezo wao wa Ligi kesho dhidi ya Dodoma Jiji FC utakao chezwa uwanja wa Jamuhuri Saa 10 jioni.

Nabi amesema hayo alipoulizwa swali kuwa amejipangaje kuhakikisha wanashinda mchezo wa kesho baada ya kucheza michezo mitatu mfululizo ilyopita bila kupata ushindi matokeo ambayo yametengeneza hofu miongoni mwa mashabiki kwenye mbio za ubingwa.

“Hatuna shaka, hatuna wasiwasi, tunaamini uwezo wa kwetu tunaamini uwezo wa wachezaji wetu. Kwenye hizo mechi 3 sio kama mpango wetu haukuwa mzuri, ni mechi ambazo tumepata nafasi nyingi za kufunga magoli lakini tulikosa bahati ya kufunga” Amesema Nasreddine Nabi

Timu ya wananchi inaongoza Ligi ikiwa na alama 57 tofauti ya alama 8 dhidi ya Simba walio nafasi ya pili wakiwa na alama 49, timu zote zikiwa zimecheza michezo 23 ikiwa imesalia michezo 7 kabla ya msimu kumalizika.

Lakini pia kuelekea mchezo huu kocha Nabi amethibitisha kuwa watamkosa kiungo wao Yannick Bangala kwenye mchezo huu. Bangala amefiwa na ndugu yake hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho. Na kocha huyo ametuma salma za pole kwenda kwa mchezaji huyo kwaniaba ya benchi la ufundi na wachezaji wote wa Yanga.A

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR WAIANDALIA SIMBA GARI LA KUBEBA WAGONJWA...OKWI NA KASEJA WATAJWA...