Home Uncategorized ALIYEWATUNGUA SIMBA NA YANGA AJICHIMBIA BUNDA KWA SASA

ALIYEWATUNGUA SIMBA NA YANGA AJICHIMBIA BUNDA KWA SASA


SIXTUS Sabilo, mshambuliaji namba moja wa Polisi Tanzania amesema kuwa kwa sasa anaendelea kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona akiwa zake nyumbani Bunda.

Akizungumza na Saleh Jembe, Sabilo amesema kuwa kwa sasa kuna mengi ambayo anayakosa kwenye mpira lakini hakuna namna ni lazima kujilinda kwanza kwani afya ni jambo la msingi.

“Kuna vitu vingi ambavyo tunavikosa kwa sasa lakini hamna namna ni lazima tukubaliane na hali na kwa sasa tunachukua tahadhari ya kulinda afya zetu kwani Virusi vya Corona vipo na ni hatari.

“Kwa sasa baada ya kambi kuvunjwa nimerejea nyumbani, Bunda ambapo nipo na familia nikiendelea kuchukua tahadhari, ninapenda kuwaomba na wengine pia wafanye hivyo kwani hali bado haijawa shwari nasi tunapenda kurejea kwenye maisha yetu ya awali,” amesema.

Wakati Ligi Kuu Bara ikisimamishwa , Sabilo alikuwaametupia mabao saba kwenye ligi kuu Bara na aliweza kuzitungua timu zote kubwa ambazo ni Yanga na Simba walipokutana.

SOMA NA HII  HESABU ZA SIMBA KWA YANGA ZIPO NAMNA HII KESHO