Home Uncategorized HESABU ZA SIMBA KWA YANGA ZIPO NAMNA HII KESHO

HESABU ZA SIMBA KWA YANGA ZIPO NAMNA HII KESHO

PASCAL Wawa beki wa Simba amesema kuwa wanapiga hesabu kubwa kuona namna gani watashinda mchezo wao mbele ya Yanga utakaochezwa Machi 8,2020, kesho Jumapili Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Pascal Wawa amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi na wao watapambana kuupata.
Wawa amesema:-: “Kazi ni kubwa na kila mechi tunaitazama kwa umuhimu wake wa kipekee ili kupata matokkeo, mechi yetu ya Yanga itakuwa ngumu ila tunazitaka pointi tatu zao,”.
Simba imefunga mabao 55, Wawa ambaye ni beki ametoa pasi moja ya bao lililofungwa na Meddie Kagere mwenye mabao 15.
SOMA NA HII  NAMUNGO: TULIWAHESHIMU YANGA