Home Uncategorized FLOYD MYWEAATHER ATAKA KUMFUNDISHA NGUMI WILDER AKAMNYOOSHE FURY

FLOYD MYWEAATHER ATAKA KUMFUNDISHA NGUMI WILDER AKAMNYOOSHE FURY


BONDIA mstaafu wa ngumi, Floyd Myweather amesema kuwa Deontay Wilder anaweza kumpiga Tyson Fury katika pambano lao la marudiano iwapo atakubali kufundishwa naye kuelekea kwenye pambano hilo.

Fury mwenye miaka 31 alimnyoosha Wilder mwenye miaka 34 kwenye pambano la uzito wa juu lililofanyika Las Vegas wiki mbili zilizopita na kuzitibua rekodi za Wilder za kutopigwa na kumpoteza mkanda wa WBC.

Pambano hilo lililoteka hisia za watu, Wilder alidondoshwa mara mbili kabla ya mwamuzi kusitisha pambano baada ya kona ya Wilder kurusha taulo raundi ya saba.

“Kama akinipa nafasi nikamfundisha basi anaweza kushinda kwenye pambano lake la marudio naweza kumpa darasa jinsi ya kushinda,” amesema Myweather.

SOMA NA HII  DILI LIKIKAMILIKA LUKAKU KUSEPA UNITED MAZIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here