Home Habari za michezo HUU NDIO UMAFIA WALIOUFANYA YANGA DHIDI YA SIMBA KWA MUSONDA…PICHA LILIANZIA HAPA..

HUU NDIO UMAFIA WALIOUFANYA YANGA DHIDI YA SIMBA KWA MUSONDA…PICHA LILIANZIA HAPA..

Tetesi za Usajili Yanga SC

Hii sasa sifa. Yanga baada ya kumnyakua kimafia kiungo Mudathir Yahya aliyekuwa hatua chache kutua Simba, jana tena mabosi wa klabu hiyo wamewaliza watani wao hao kwa kuwapora straika waliyekuwa wakimpigia hesabu kumbeba ili azibe nafasi ya Cesar Manzoki.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ndiye aliyehusika na umafia huo baada ya kupanda ‘pipa’ kimya kimya na kwenda Zambia kumfuata straika mmoja hatari mwenye mashuti makali, Kennedy Musonda ambaye alikuwa akinyemelewa na Simba na hadi jioni ya jana asilimia 99 ya dili lilitiki.

Habari zinasema kwamba Yanga ilishamalizana na nyota huyo wa Zambia anayekipiga timu ya Power Dynamos ya nchini humo.

Hii ikiwa siku moja tangu , kocha Nasreddine Nabi kuutaka uongozi kumleta mtupia nyavuni mkali wa kusaidiana na Fiston Mayele kutoka DR Congo.

Tayari mkataba wa miaka miwili wa Musonda ulikuwa mezani tayari kwa ajili ya kuja kuvaa jezi za njano za Yanga kama klabu anayotoka ya Dynamos.

Usajili huo umetokana na kupata taarifa za ubora wa mshambuliaji huyo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Andre Mtine ambaye alifanya kikao cha haraka na kocha Nabi aliyekuwa akisisitiza anataka straika na beki mmoja afunge usajili katika dirisha dogo na kisha uamuzi ukafikiwa.

Baada ya Nabi kupitisha usajili huo, haraka Hersi alisafiri hadi Zambia kumaliza dili hilo hasa baada ya kushtuliwa kwamba watani wao Simba nao walikuwa wakimpigia hesabu kali mshambuliaji huyo.

Simba ilikuwa inamtaka Musonda ambaye ana urefu wa mita 1.76 kuja kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya kuona kumpata Cezar Manzoki kuna safari ngumu.

Hersi pia kumnasa Musonda ni kuwajibu Simba ambao mwaka 2020 walimpiga bao baada ya kuiwahi Yanga wakimsajili kiungo Larry Bwalya ambaye alikuwa ameshakubaliana kila kitu na mabingwa hao wa nchi.

Hata hivyo, kupitia fedha za bilionea wao Mohamed Dewji fasta wekundu hao walipindua dili wakiwapa fedha nyingi Dynamos katika kununua mkataba wa kiungo huyo.

Musonda aliyezaliwa Desemba 22, 1994 amewahi kucheza klabu mbalimbali za nchi kwao ikiwamo Lusaka Dynamos, Zanaco, Nakambala Leopards na Green Eagles.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA USAJILI WA MNIGERIA ETOP DAVID UDOH KUJIUNGA SIMBA IKO HIVI...KUMBE NAYE NI WALEWALE TU....

1 COMMENT