Home Habari za michezo BAADA YA KUONA ‘PYEPYE’ ZA PABLO ZIMEKUWA NYINGI…SIMBA WAMPA WIKI TU KUHAMUA...

BAADA YA KUONA ‘PYEPYE’ ZA PABLO ZIMEKUWA NYINGI…SIMBA WAMPA WIKI TU KUHAMUA HATMA YAKE MSIMBAZI…


Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco amepewa wiki moja kuandaa ripoti maalumu kwa ajili ya masuala ya kiufundi kabla ya msimu ujao kuanza mambo gani anayotaka yafanyike kufanya vizuri.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zinasema kwamba viongozi wamemwambia Kocha huyo awape kila kitu anachokifikiria lakini pia awaweke wazi nini hatma yake. Simba imepania kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao unaoanza mwishoni mwa mwaka huu.

Viongozi hao wamekiri kuzizisikia taarifa za kocha wao kuhitajika na Orlando Pirates ya Afrika Kusini ingawa wamedai kuwa kocha hajawapa taarifa rasmi.

“Sisi tumemwambia atupe ripoti ambayo itaendana na matakwa yake na kama pia hatakuwepo atuandae mapema ili tujue tunaandaaje timu, kwasababu hatuwezi kuandaa timu kwa programu yake halafu anakuja kocha mwingine ambaye ni vitu viwili tofauti,” alidokeza kiongozi mmoja wa Simba.

Hata hivyo, Pablo alisema hawezi kuitolea ufafanuzi taarifa isiyokuwa rasmi hasa kuhusu hatma yake ya msimu ujao.

“Muda sahihi wa kujibu suala hilo utakapofika nitakujulisha, ila nafahamu ligi ya Afrika Kusini ni kubwa na nzuri,” alisema Pablo akizungumzia suala hilo.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUKOSA MAGOLI JUZI...KAGERE APEWA HESABU YA MAGOLI 15 KWA MSIMU HUU....HANS PLUIJM ABAKI KUCHEKA TU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here