Home Uncategorized PAUL POGBA AIKAZIA MANCHESTER UNITED, KUOMBA ASEPE ZAKE MSIMU UJAO

PAUL POGBA AIKAZIA MANCHESTER UNITED, KUOMBA ASEPE ZAKE MSIMU UJAO

IMERIPOTIWA kuwa Paul Pogba kiungo wa Manchester United ana mpango wa kuwaomba mabosi zake wampe ruhusa ya kuondoka ndani ya kikosi hicho kabla hawajafanya ziara ya kwenda Australia.
Pogba kwa sasa amekuwa hana mpango wa kubaki ndani ya United baada ya kusema kwamba anahitaji kupata changamoto mpya nje ya kikosi hicho.
Real Madrid na timu yake ya zamani ya Juventus zote imeripotiwa kwamba zinaiwinda saini ya nyota huyo ambaye Taifa lake la Ufarasa limetwaa kombe la Dunia.
SOMA NA HII  SAMATTA SASA KUKUTANA NA MANCHESTER CITY AMA MANCHESTER UNITED FAINALI YA CARABAO