Home kimataifa KISA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA…AL MERRIKH YA SUDANI WAMSHITAKI KOCHA WA AL...

KISA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA…AL MERRIKH YA SUDANI WAMSHITAKI KOCHA WA AL AHLY YA MISRI..


Makamu wa Rais wa Al Merreikh, Adel Abugreisha amesema kuwa kitendo cha kocha wa Al Ahly inayoshiriki mashindano ya klabu bingwa, Pitso Mosimane kuhusika katika kuendesha droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika inaleta mgongano wa kimaslahi.

“Tulipeleka malalamiko yetu kwenye Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupitia barua rasmi, kupitia kwa Rais Hazem Mostafa, kwa sababu ya Mosimane kuchaguliwa kuwa kwenye timu ya watu waliochezesha droo ya Ligi ya Mabingwa na hatujapata majibu kutoka CAF hadi sasa,” amesema Abugreisha.

SOMA NA HII  WAKATI LIGI ZIKIWA ZIMESIMAMA DUNIANI KOTE...DStv BADO WAKO NA WEWE...NA SAFARI HII NI KWA AFCON YA WANAWAKE ...