Home Uncategorized BALAA LA SALAH LIPO NAMNA HII UWANJANI, KOCHA MKUU ATOA NENO

BALAA LA SALAH LIPO NAMNA HII UWANJANI, KOCHA MKUU ATOA NENO


MOHAMED Salah, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Liverpool ametumia dakika 2,246 kabla ya Ligi Kuu England kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Ametupia jumla ya mabao 16 na ametoa pasi sita ndani ya Ligi Kuu England.Ana wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 140.


Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa ni miongoni mwa wachezaji makini ambao wanatumia akili ndani ya uwanja.

“Anapenda kufanya vizuri akiwa ndani ya uwanja ambapo anatumia akili na nguvu pia, ni wakati ambao tunapenda kuona namna gani ataendelea kulinda kipaji chake,” amesema.

Ligi Kuu England kwa sasa imesimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.

SOMA NA HII  AZAM FC YAANZA KUIWINDA SIMBA, YAPANIA KUFANYA MAAJABU