Home Uncategorized BEKI SIMBA ATAKA KUCHEZA YANGA

BEKI SIMBA ATAKA KUCHEZA YANGA

ZANA Coulibaly, raia wa Ivory Coast amesema kuwa yupo tayari kurejea Bngo kukipiga ndani ya Yanga iwapo watahitaji huduma yake.
Beki huyo alidumu Simba kwa miezi tisa kabla ya kuondoka na kujiunga na AS Vita ya DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili katika michuano ya kimataifa amefanikiwa kucheza mechi tatu pekee msimu huu.
Coulibaly amesema kuwa moja kati ya sehemu ambazo hawezi kuzisahau kirahisi ni Tanzania na yupo tayari kurejea kwa kujiunga na timu yoyote zikiwemo Azam na Yanga kutokana na ukarimu wa watu wake.
“Tanzania kiukweli nilikuwa na furaha kwa sababu watu wake ni wakarimu na wanawajali wengine, ukiangalia katika mechi mashabiki wanajitokeza kwa wingi na wakati wote wanashangilia kitu ambacho ni nadra kukiona katika mataifa mengine ya Afrika, bado nawakumbuka sana.
“Natamani kuona narudi tena huko kucheza haijalishi ni timu gani iwe kama Azam au hata Yanga wakinihitaji nitakuwa tayari kurejea,” amesema Coulibaly.
SOMA NA HII  DUBE ATAKATA AZAM FC IKIPIGA 4G