Home Uncategorized KMC KUONGEZA MASHINE MOJA YA KAZI

KMC KUONGEZA MASHINE MOJA YA KAZI


KOCHA wa KMC, Haruna Harerimana yenye maskani yake Kinondoni amesema kuwa anahitaji kupata saini ya mlinda mlango mpya atakayeongeza changamoto ndani ya kikosi chake.

KMC imekuwa na makipa wawili ambao wanachezea timu ya Taifa ikiwa ni pamoja na Jonathan Nahimana anayedakia timu ya Taifa ya Burundi na Juma Kaseja ambaye ni kipa ndani ya Timu ya Taifa ya Tanzania.

Kocha huyo amesema makipa wake wote ni bora ila anahitaji kuwapa changamoto mpya.

“Haina maana kwamba hawa waliopo hawafai hapana wapo vizuri imani yangu ni kuona kwamba kila mmoja anazidi kuwa makini.

“Watakaokuja itakuwa kwamba kipa atakayekuja ataongeza nguvu na nafasi ya kuchagua nani aanze kikosi cha kwanza,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA WATUA KWA BEKI WA KIMATAIFA,TONOMBE, CARLINHOS WALISHWA KIAPO,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI