Home Uncategorized BEKI RUVU SHOOTING AJIWEKA SOKONI

BEKI RUVU SHOOTING AJIWEKA SOKONI

BEKI wa kati wa timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani Santos Mazengo amesema kuwa, kwa sasa yupo huru kufanya mazungumzo na timu yoyote kwa kuwa mkataba wake na timu hiyo unaisha mwishoni mwa msimu huu.

     Mazengo ameongeza kuwa, anaikaribisha timu yoyote inayohitaji huduma yake kufanya nayo mazungumzo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi
        Mazengo aliyesajiliwa na Ruvu Shooting misimu miwili iliyopita akitokea kikosi cha vijana cha timu hiyo amekuwa katika kiwango kikubwa msimu huu na ameweza kuisadia timu yake kwa kiwango kikubwa.
      Aidha mchezaji huyo amesema kuwa anaipa nafasi ya kwanza timu yake ya Ruvu Shooting kufanya mazungumzo naye kama watataka kuendelea kupata huduma yake.
      “Kwa sasa nipo huru kufanya mazungumzo na timu yoyote kwani mkataba wangu unaisha mwishoni mwa msimu huu, hivyo nazikaribisha timu zozote zinazohitahiji saini yangu”,alisema Mazengo
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA