Home Uncategorized BEKI WA COASTAL UNION AZIPASUA KICHWA SIMBA NA YANGA

BEKI WA COASTAL UNION AZIPASUA KICHWA SIMBA NA YANGA


BAKARI Mwamnyeto, beki wa Coastal Union ameziingiza vitani timu za Kariakoo, Simba na Yanga ambazo zote zinaisaka saini yake.

Mwamnyeto amekuwa kwenye hesabu kali na mabosi wa Simba ambao wanahitaji kuongeza nguvu kikosini hapo kwa ajili ya msimu ujao.

Habari zinaeleza kuwa tayari mabosi wa Yanga wameingia kwenye mpango wa kuinasa saini yake ili kumuongezea nguvu Lamine Moro na Kelvin Yondani.

Mussa Kassa, meneja wa beki huyo amesema kuwa amepata dili nyingi zinazomtaka beki huyo ikiwa ni pamoja na Simba na Yanga.

“Simba na Yanga wamekuwa kwenye mpango wa kumpata beki wa Coastal Union ila nimewaambia kwamba ikiwa wapo siriaz wazungumze na Coastal Union ambao wao ndio mchezaji wao kwa sasa.

“Kuhusu gharama za mchezaji na dau lake siwezi kuliweka mezani kwa sasa kwani ni suala la makubaliano,” amesema.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA APEWA MBINU YA KUIMALIZA FC PLATINUM LEO