Home Habari za michezo PABLO AKAZIA ISHU YA SIMBA KUWA NA KIPORO KISA MECHI NA WASAUZI…AMWAGA...

PABLO AKAZIA ISHU YA SIMBA KUWA NA KIPORO KISA MECHI NA WASAUZI…AMWAGA ‘DATA’ HADHARANI…

 Kocha mkuu wa Simba Pablo Franco amesema aliwaomba viongozi wa klabu hiyo kuomba mchezo wao wa hatua ya robo fainali wa kombe la FA dhidi ya Pamba ya Mwanza kusogezwa mbele ili wapate muda mzuri wa kujiandaa na mchezo dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.


Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kiporo dhidi ya timu ya Polisi Tanzania kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi hapo kesho ,Pablo amesema hilo lilikuwa ombi lake ili kupata nafasi ya muda mwingi wa kujiandaa kwani wamekuwa na ratiba ngumu inayowakabili kwa sasa .

β€œkama kocha niliongea na viongozi kuomba mchezo wetu uhairishwe kidogo kwa sababu hatuchezi kama klabu zaidi ya kuwakilisha taifa, unajua kwa timu iliyowahi kufika fainali miaka 30 iliyopita na sasa ina nafasi ya kufanya hivyo tunapaswa kuwa na maandalizi mazuri mana tungeamua kucheza kulikuwa na mambo mawili tubadilishe wachezaaji wa kikosi cha kwanza au tuwatumie huku tukiomba wasipate majeraha kwenye mchezo kitu ambacho hujui kitu gani kinaweza kutokea β€œamesema Pablo

Simba watakuwa na kibarua pevu dhidi ya Orlando Pirates kwenye michezo miwili ya mkondo wa robo fainali mnamo tarehe 17 na 24 April,2022 huku taarifa njema ni kuruhusiwa kwa mashabiki elfu 60,000 kuingia kwenye mkondo wa kwanza utakaofanyika kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku mchezo huo ukihusisha teknolojia ya VAR.

SOMA NA HII  GAMONDI ATAJA SABABU ZA KUPOTEZA MCHEZO WAO KIMATAIFA...... AL AHLY YATAJWA HUKU WACHEZAJI WAKIPEWA NENO HILI