Home Habari za michezo AZIZ KI AFUNGUKA “UCHAWI” ULIOMFANYA ARUDI ‘MJINI’ NA YANGA MSIMU HUU…

AZIZ KI AFUNGUKA “UCHAWI” ULIOMFANYA ARUDI ‘MJINI’ NA YANGA MSIMU HUU…

Habari za Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki kwa msimu huu ameanza na moto, kiasi cha kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo, lakini mwenyewe amefichua zinazombeba huku akiweka bayana namna alivyojipanga kuendelea na kasi aliyoanza nayo arejeshe fadhila Jangwani.

Aziz Ki ambaye alisajiliwa msimu uliopita akitokea ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast ameanza msimu huu vizuri kwa kufunga takribani kilaechi anayocheza tofauti na msimu wa mwaka jana alipokuwa akijiunga na Wananchi jambo ambalo limefufua matumaini mapya kwa mchezaji huyo.

“Msimu uliopita sikuwa bora nilipambana, lakini sikufikia lengo la mashabiki na viongozi nimejitafakari na nimeweza kujitafuta na kujipata mwanzo wangu umekuwa bora natamani kumaliza vizuri zaidi ili kukata kiu ya wanayanga walioniamini na kunisajili.

“Ubora nilionao unatokana na namna timu ilivyosajiliwa sio rahisi kukaa kujisahau wakati kuna wachezaji wazuri kwenye namba ninayocheza napambana kuhakikisha nakuwa bora na naipambania timu kutetea mataji yaliyobaki,” amesema Aziz.

SOMA NA HII  KAPITISHA MWAKA NCHIMBI BILA KUFUNGA, SAWA, LAKINI TUSIISHIE KUMCHEKA