Home Habari za Yanga Leo GAMONDI ACHIMBA MKWARA…YANGA YAVUNA MABILIONI

GAMONDI ACHIMBA MKWARA…YANGA YAVUNA MABILIONI

habari za yannga

KLABU ya Yanga imejihakikishia Sh30 milioni kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia za ‘Bao la Mama’, pia baada ya kutinga makundi imejihakikisha Dola 700,000 (zaidi ya Sh 1.8 bilioni) kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo ya CAF.

Yanga sasa inaigeukia Ligi Kuu Bara ambapo Jumatano itaifuata KenGold jijini Mbeya, huku kocha  Gamondi akipiga mkwara akisema kwa sasa wao ni mwendo mdundo tu hadi kieleweke.

Kocha huyo aliyetwaa taji la ligi msimu uliopita ikiwa ni msimu wa kwanza tangu ajiunge na Yanga, aliliambia Mwanaspoti anataka kuona kila nafasi wanayoipata inageuzwa kuwa bao kwani tayari amewapa mbinu bora wachezaji.

Raia huyo wa Argentina, alibainisha kuwa mchezo wa jana dhidi ya CBE aliingia kama sehemu ya kuangalia kile alichofundisha kama kimeanza kufanya kazi, akipanga kuendeleza balaa hilo katika ligi.

Ikumbukwe katika raundi tano za ligi hadi sasa, Yanga ndiyo timu pekee iliyocheza mechi moja tu na ilianza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar na sasa itakuwa zamu ya kuvaana na KenGold iliyopanda daraja msimu huu..

“Naamini kwa sasa kiwango chetu cha kufunga mabao kinaendelea kuimarika, imani yangu ni tutazidi kuwa bora katika mechi zilizo mbele yetu.

“Malengo ni kutaka kuona kila nafasi tunaigeuza kuwa bao kwani hakuna timu inayopata ushindi bila ya kufunga mabao, wachezaji wangu wanalielewa hilo,” alisema Gamondi ambaye msimu uliopita aliifikisha Yanga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO DABI...SURE BOY ATULIZA PRESHA YANGA...NABI ROHO KWATUU..