Home Habari za michezo BAADA YA KUPOA MAUMIVU YA KIPIGO CHA WAIVORY..PABLO KWA MARA YA KWANZA...

BAADA YA KUPOA MAUMIVU YA KIPIGO CHA WAIVORY..PABLO KWA MARA YA KWANZA AJA NA HILI JIPYA…


KUELEKEA mchezo wao wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa watafanya kila kinachowezekana kushinda mchezo huo, ili kutinga hatua ya robo fainali.

JUMAPILI ya Aprili 3, mwaka huu, Simba wanaokamata nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi D, wanatarajia kuwa wenyeji wa USGN katika mchezo huo wa sita wa hatua ya makundi unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

SIMBA ambao mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya pointi saba katika michezo yao mitano waliyocheza, wanatakiwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya USGN ili ku[1]jihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.

AKIZUNGUMZA na gazeti la michezo la  Championi Ijumaa, kocha Pablo alisema: “Tulitamani kupata matokeo katika mchezo wetu uliopita dhidi ya ASEC Mimosas ili tusiwe kwenye presha kubwa katika mchezo huu wa mwisho dhidi ya USGN, lakini haikuwa hivyo. “Hayo yamepita na kazi kubwa iliyo mbele yetu kwa sasa ni kuhakikisha tunashinda mchezo ujao na kutinga robo fainali, tunacheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu na hatima ya kufuzu kimchezo iko mikononi mwetu, hivyo tutafanya kila linalowezekana kufanikisha hilo kwa kuwa tunaamini hakuna sababu ya kushindwa.”

SOMA NA HII  FT: RUVU SHOOTING 1-3 SIMBA SC....KAGERE ATAKATA..KIBU DENIS AONA 'MWEZI'....