Home Habari za michezo MSUVA TENA…AFUNGUKA ISHU YA KUTAKIWA NA TIMU ‘CHUNGU LAKI’ …AWATULIZA KIMTINDO WATZ…

MSUVA TENA…AFUNGUKA ISHU YA KUTAKIWA NA TIMU ‘CHUNGU LAKI’ …AWATULIZA KIMTINDO WATZ…


MSHAMBULIAJI wa Taifa Stars, Simon Msuva, amesema kuwa Watanzania na mashabiki wake wasiwe na hofu juu ya kiwango chake kwani muda siyo mrefu atapata timu ya kuchezea kutokana na timu nyingi kuonyesha nia ya kumhitaji.

Msuva alisema yupo mbioni kujiunga na moja ya timu ambazo zinamhitaji kwa ajili ya kuanza kufanya nayo mazoezi, ili kutekeleza agizo la Kocha wa Stars, Kim Poulsen, ambaye alimtaka kutafuta timu kwa ajili ya kulinda kiwango chake.

Msuva alisema amepokea ofa nyingi kwenye meza yake, huku akigoma kuzitaja kwa majina na nchi zinapotoka, huku akisimamia kauli yake ya Watanzania wasiwe na hofu watamuona akiwa na timu na suala lake litaisha. “Watanzania wasiwe na hofu suala langu litaisha tu na muda siyo mrefu nitapata timu ya kufanyia mazoezi kwa sababu zipo nyingi sana ambazo zinanihitaji,” alisema Msuva.

Msuva alirejea Tanzania takriban miezi mitatu iliyopita akigoma kuitumikia klabu yake ya Wydad Casablanca ya Morocco akishinikiza kupewa stahiki zake. Na suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na Fifa.

SOMA NA HII  ILE SINEMA YA MPOLE NA MABOSI ZAKE...YAFIKIA HATUA HII...GEITA WAKIMBILIA INSTGRAM...