Home Habari za michezo KISA NGAO YA JAMII KUPIGWA TANGA…JEMEDARI AMVAA KARIA…AFUNGUKA ANAVYOPENDELEA KWAO..

KISA NGAO YA JAMII KUPIGWA TANGA…JEMEDARI AMVAA KARIA…AFUNGUKA ANAVYOPENDELEA KWAO..

Habari za Simba

Mchambuzi wa masuala ya soka, Jemedari Said amemvaa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kufuatia maamuzi ya shirikisho hilo kupeleka mechi za Ngao ya Jamii kwenda kuchezwa katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

jemedari amesema kuwa haoni sababu ya kupeleka mechi hizo Tanga kwani ni upendeleo hasa ikizingatiwa kuwa hivi karibuni mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na Azam ulipigwa uwanjani hapo.

“Kwanza kwa nini Tanga, wakati hata fainali ya FA uwanja haukujaa, mimi sioni sababu maalum mashindano haya kupelekwa Tanga, kwangu naona ni upendeleo, Rais analeta upendeleo mechi zote kupelekwa Tanga.

“Tanga sio kiwanja bora cha kucheza, ukitoa Kwa Mkapa basi ni Chamanzi, na mbona Kiwanja cha Chamanzi kipo tu, yeye Rais Karia anasema Tanga ni karibu, hakuna lolote huu ni upendeleo tu,” amesema Jemedari Saidi.

Habari Zinazofanana:

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA TP MAZEMBE...THOMAS ULIMWENGU AILENGESHEA YANGA...AANIKA SIRI ZA WACONGO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here