Home Yanga SC YANGA: BADO HATUJAMALIZA LIGI, WAKUMBUSHIA ISHU YA MWADUI

YANGA: BADO HATUJAMALIZA LIGI, WAKUMBUSHIA ISHU YA MWADUI


 RAZACK Siwa, Kocha wa Makipa wa Yanga amesema kuwa bado hawajamaliza ligi hivyo mchezo wa leo dhidi ya Ihefu watapambana kupata pointi tatu.

Yanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ihefu mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.

Walipokutana mara ya kwanza Uwanja wa Sokoine ubao ulisoma Ihefu 0-3 Yanga.

Siwa amesema kuwa bado hawajamaliza ligi hivyo watapambana kupata pointi kwenye mchezo huo.

“Wengi wanafikiri ligi imeisha sisi bado tupo kazini na mchezo wetu dhidi ya Ihefu tutapambana kupata pointi tatu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

“Kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo hivyo ni wakati wetu wa kuona kwamba tunashinda. Ipo wazi kwamba mchezo wetu dhidi ya Ihefu utakuwa mgumu hasa ukizingatia kwamba ipo kwenye nafasi ya kushuka daraja.

“Tunakumbuka tulipokutana na Mwadui FC ambayo imeshuka daraja tulipata tabu kushinda dakika za lala salama,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya pili na pointi 70 inakutana na Ihefu iliyo nafasi ya 15 na pointi 35 ikiwa inapambana kujinasua kwenye nafasi ya kushuka daraja.

Pia mchezo wa leo utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kusema asante kwa nyota wao Haruna Niyonzima ambaye kandarasi yake imemeguka na hataongeza mkataba mwingine.

SOMA NA HII  SAFARI YA KAMBI MAREKANI YAZIDI KUNUKIA YANGA....GSM AGOMA KURUDIA YA MOROCCO MWAKA JANA...