Home Habari za Yanga Leo YANGA YATINGA MAKUNDI CAF KWA REKODI YA KIBABE…CHAMA ANAKIMBIZA TU

YANGA YATINGA MAKUNDI CAF KWA REKODI YA KIBABE…CHAMA ANAKIMBIZA TU

HABARI ZA YANGA-CHAMA

HISTORIA imeandikwa tena Kibabe usiku wa jana Yanga ikitinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya pili mfululizo ikiing’oa CBE SA ya Ethiopia, huku Clatous Chama akiendelea kung’ara katika michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Yanga ikicheza kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, ilipata ushindi wa mabao 6-0 na kuitupa nje CBE kwa jumla ya mabao 7-0 baada ya awali kushinda ugenini bao 1-0 wiki iliyopita.

Yanga imetinga hatua hiyo ya makundi kwa rekodi ya aina yake ya kufunga jumla ya mabao 17-0 kwani katika mechi za raundi ya awali iliishinda Vital’O ya Burundi kwa jumla ya mabao 10-0.

Kocha Miguel Gamondi aliyeirejesha Yanga makundi msimu uliopita baada ya kupita miaka 25 na kwenda kung’olewa robo fainali, jana aliendeleza rekodi hiyo na kuwapa furaha Wanayanga.

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI HUYU AWAOGOPA WANANCHI..."HAKUNA KITU KIGUMU KAMA KUCHEZA NA YANGA