Home news LALA SALAMA NI MUDA WA MAPAMBANO, SHERIA 17 ZIFUATWE

LALA SALAMA NI MUDA WA MAPAMBANO, SHERIA 17 ZIFUATWE


NGOMA inapigwa kwa kasi kwenye ligi kwa sasa ikiwa ni mzunguko wa pili na kila mmoja anapigania malengo yake ili kupata kile anachostahili.

Bado vita ya ubingwa ni mbichi kwa sasa ambapo zile zilizo tatu bora zinapewa nafasi ya kumtoa mbabe ambaye atasepa na taji hilo lenye thamani kubwa kwa timu.

Vinara Simba na Yanga wanavutana kasi huku Azam FC ikiwa namba tatu kwenye msimamo.

Ipo wazi kwamba bingwa mtetezi ambaye ni Simba naye malengo yake ni kuona anaweza kutetea taji hilo huku Yanga nao wakiweka wazi kwamba wanahitaji kulitwaa taji hilo baada ya kulikosa kwa muda mrefu.

Azam FC pia wao mdogomdogo wanasema kwamba wana jambo lao ambalo wanahitaji kutimiza hivyo kwa kuwa kila mmoja ana mechi mkononi ni suala la kusibiri na kuona.

Kama ilivyo ngumu kwenye ubingwa pia ni ngumu kwenye kushuka daraja pamoja na zile ambazo zitamaliza ndani ya 10 bora mchakato ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi.

Kwa sasa kila timu inajipanga kuja kufanya vizuri ndani ya uwanja na kupata matokeo.

Huu ni mpira na kila timu inastahili kushinda hivyo hakuna timu ambayo inapaswa kufungwa wala ambayo inapaswa kushinda muda wote.

Mwadui kwa sasa habari yao ni kufikiria Ligi Daraja la Kwanza ila ninawapa neno kwamba walikuwa na kazi ya kuanza kwa gia ya upambanaji tangu awali.

Tunajua kwamba uchumi ni tatizo kubwa linalosumbua timu zetu ila kuna mechi nyingine walikuwa wanajitoa na nyingine wanacheza kukamilisha ratiba.

Kumbuka pia waliweza kucheza vizuri pia mbele ya Azam ambayo nayo ipo ndani ya tatu bora maana yake ni kwamba kila kitu kwenye soka kinawezekana kama ambavyo walicheza vizuri mbele ya Simba.

Jambo kubwa ambalo ningependa lifanyike katika mechi hizi za mwisho ni lazima kuwe na usawa na mechi zichezwe kwa kufuata sheria 17 za mpira.

Mtu ashinde kwa kutumia nguvu zake mwenyewe na hakuna ujanjanja ambao utafanyika kwani tunahitaji kuona kwamba kila kitu kinakwenda sawa.

SOMA NA HII  MASHABIKI WA SIMBA WANAVYOTESEKA NA SOKA LA ROBERTINHO

Lala salama kwa timu zote iwe ni ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi Daraja la Kwanza ni muhimu kuweza kuona kwamba kila timu inashinda kwa haki. 

Katika hili ipo wazi kwamba ni jambo la msingi kupata mshindi ambaye hatapata tabu akipanda ligi msimu ujao wa 2021/22 itasaidia kueleta ushindani mkubwa .

Kwa kuwa hizi ni mechi za mwisho na zina umuhimu mkubwa kwa kila timu kupata matokeo mazuri ambayo yatawafanya wafikie malengo waliyojiwekea.

Kikubwa kinachotakiwa kwa sasa ni kuona kwamba kila timu inafanya maandalizi mazuri ili kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja ambayo yatawapa kile ambacho wanakihitaji. 

Wapo ambao wamekuwa wanapenda kuleta ugomvi ndani ya uwanja hayo yamepitwa na wakati ni muhimu kutulia na kufanya maamuzi kwa akili zaidi.

Hivyo wale wote ambao watakuwa uwanjani wapambane kutafuta matokeo ndani ya uwanja kupata matokeo chanya.