Home Habari za michezo EDO KUMWEMBE AWATOLEA UVIVU SIMBA SC KUHUSU KUWEKA KAMBI UTURUKI…. ISHU IKO...

EDO KUMWEMBE AWATOLEA UVIVU SIMBA SC KUHUSU KUWEKA KAMBI UTURUKI…. ISHU IKO HIVI

Mchambuzi nguli wa masuala ya Soka nchini, Edo Kumwembe amedai kuwa kikosi cha Klabu ya Simba kilikwenda nchini Uturuki kuzurura tu badala ya kujiandaa na msimu mpya wa soka.

Haya ni maoni ya Edo kufuatia kiwango alichokiona kwa Simba katika mechi zake za hivi karibuni kuanzia mchezaji mmoja mmoja mpaka kikosi kizima.

“Klabu ya Simba SC walijifungia Uturuki lakini ukweli ni kwamba hatukuona maajabu ya kambi yao ya Uturuki hatujui kocha wao, Robertinho anataka nini katika kikosi.

“Kinachojulikana ni kwamba Simba bado hawapo tayari kwa msimu mpya wa michuano mbalimbali. Juzi tukagundua kwamba mchezaji aliyesubiriwa na wengi katika soka letu, Jose Luis Miquissone naye ana kazi ndefu ya kuwa fiti na kurudi katika kiwango.

“Mpaka sasa ni mchezaji wa kawaida tu na sio yule aliyeondoka nchini akiwa tishio, ana kazi kubwa ya kufanya,” Edo Kumwembe.

Una maoni gani kuhusu hili?

SOMA NA HII  HII SASA NDO INAITWA SIMBA NA MKATABA WA BALEKE....... NI UMAFIA TU