Home Habari za michezo KUHUSU YANGA KUJAZA UWANJA RWANDA, WACHAMBUZI WASEMA HAYA

KUHUSU YANGA KUJAZA UWANJA RWANDA, WACHAMBUZI WASEMA HAYA

KOCHA AS VITA SALUTI...KUWAVUSHA YANGA NUSU FAINALI SHIRIKISHO

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa Klabu ya yanga wanao uwezo wa kuujaza Uwanja wa Pele mjini Kigali nchini Rwanda kwa sababu wanao mashabiki wa kutosha nchini humo.

Wakanda amesema hayo kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo yanga atakipiga na Al-Merreikh ya Sudan mnamo Septemba 16, nchini Rwanda.

“Yanga wakienda nchini Rwanda wana uwezo wa kuujaza uwanja kwa sababu Wanyarwanda wengi wamekuwa wakiifuatilia Ligi ya Tanzania kwa sasa, na wanazishabikia hizi timu zetu mbili kati ya Simba na Yanga, kwahiyo hilo ni eneo ambalo Yanga anaenda kufaidika akiwa nchini Rwanda.

“Na ndio maana last week Al-Merrikh walipeleka barua CAF wakiomba mechi yao dhidi ya Yanga iondolewe nchini Rwanda ipelekwe nchini Morocco lakini CAF wakapinga hilo ombi, na mechi ikabaki nchini Rwanda,” amesema Wakanda Republic.

Yanga wamepanga kuondoka nchini Septemba 14, 2023 kuwafuata Wasudan ambao wamechagua Rwanda kuwa ndiyo Uwanja wao wa nyumbani kufuatia hali ya amani kuwa mbaya nchini mwao.

SOMA NA HII  KUMBE MASTAA HAWA NDIO WANAMPA KIBURI GAMONDI