Home Habari za michezo SIMBA WAWACHARUKIA YANGA KISA HIKI HAPA

SIMBA WAWACHARUKIA YANGA KISA HIKI HAPA

Habari za michezo

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema watani wao Yanga SC, wamemuiga kwa kuanzisha utaratibu wa kusafirisha mashabiki kwa njia ya basi mechi za nje ya nchi.

Ahmed ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya Simba kutangaza kuwa watawasafirisha mashabiki kwa basi kwenda nchini Zambia watakapocheza na Power Dynamos na kisha Yanga nao kufuata wazo hilo kwa kutangaza safari yao kwenda Rwanda kuwavaa Al-Merrikh SC.

“Nilianzisha Utamaduni wa kusafiri na Mashabiki Nje ya Nchi kwa kutumia Bus, Naambiwa Nyuma Mwiko Wameigaa. Endeleeni tu kutumia akili yangu na endeleeni tu ku copy mambo ya Simba, siku nikiacha kufikiria mtalia sana,” alisema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  NABI AFUNGUKA KUHUSU MBINU ZA KOCHA MPYA SIMBA..ADAI NI BORA GOMES.." HUYU KAZI KUKABA TU"