Home Habari za michezo MAXI NZEGELI YAMKUTA YA MAYELE YANGA

MAXI NZEGELI YAMKUTA YA MAYELE YANGA

Habari za Yanga

Mchambuzi mbobezi wa michezo kutoka EFM, Jemedari Said Kazumari amesema kuwa kiungo wa Klabu ya Yanga, Max Mpia Nzengeli yupo Yanga kwa mkopo akitokea AS Maniema ya Congo DR.

Jemedari amesema ana uthibitisho wa anachokisema akisisitiza kuwa yupo kwa Mkopo kama ambavyo Fiston Mayele alikuwa kwa mkopo Yanga.

“Simba walijaribu kumchukua Max wakashindwa, mimi najua. Ishu ilikuwa makubaliano tu, Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kumuulizia, baadaye wakaja Simba, lakini wakati wanataka kumchukua Yanga wakawahi wakamalizana na kumchukua.

“Sio kumalizana kwa maana gani, Max ni mchezaji wa mkopo hivyo walimalizana kwa makubaliano ya kimkopo. Wachezaji wengi wa Congo wapo Tanzania kwa mkopo, Max ni mchezaji wa mmkopo kama alivyokuwa Fiston Mayele.

“Nina uhakika kwa sababu mpaka ITC ilipotoka ninajua na uhamisho wa Mayele ulihusisha klabu tatu,” amesema Jemedari Said.

Max ameonyesha uwezo mkubwa tangu atue Yanga msimu huu akiwa amecheza mechi sita na kufunga mabao manne na assist nne.

SOMA NA HII  YANGA KUMTAMBULISHA STAA WAO HUYU MPYA