Home Habari za michezo PAMOJA NA KUSAJILIWA KWA MBWEMBWE ZOTE….KAMBOLE, MORRISON WAPEWA MIEZI MITATU YANGA….NABI AANDA...

PAMOJA NA KUSAJILIWA KWA MBWEMBWE ZOTE….KAMBOLE, MORRISON WAPEWA MIEZI MITATU YANGA….NABI AANDA RIPOTI….


LICHA ya kucheza mechi mbili za kimashindano, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi,  amesema kwa sasa babo hawezi kutoa tathimini ya ubora wa wachezaji wake wapya na badala yake anawapa muda wa miezi miwili hadi mitatu.

Wachezaji wapya wa Yanga ambao imewasajili msimu huu ni Aziz Ki raia wa Burkina Faso, Mrundi Gaël Bigirimana, Mghana Bernard Morrison, Joyce Lomalisa (DR Congo) na Lazarous Kambole raia wa Zambia ambaye hajacheza mechi hata moja ya mashindano.

Mchezo wa kwanza wa mashindano, Yanga iliibuka na ushindi mabao mawili dhidi ya Simba kwenye Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi iliyopita kabla ya juzi kupata matokeo kama hayo dhidi ya Polisi Tanzani katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu msimu huu iliyopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha shukran kwa Fiston Mayele na Bakari Mwamnyeto waliocheka na nyavu.

Nabi alisema kutokana na kutopata maandalizi mazuri ya msimu mpya (Pre-Season), hawezi kutoa tathmini ya wachezaji wake wapya na anawapongeza nyota wake kwa kupambana kutafuta matokeo.

“Kwa sasa ni mapema kutoa tathmini za wachezaji wangu wapya na nimewapa muda wa miezi miwili hadi mitatu baada ya hapo ndiyo naweza kutoa tathimini kwa sababu watakuwa wameshazoeana na kutengeneza muunganiko mzuri na wachezaji waliowakuta,” alisema Nabi.

Kuhusu mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, alisema ulikuwa mgumu na kwamba misimu yote wanapokutana na Polisi Tanzania inakuwa mechi ngumu kutokana na wapinzani wao hao kucheza soka la kujilinda zaidi.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA LWANGA KUBAKI AU KUTUPIWA VIRAGO SIMBA IKO HIVI...DAKTARI WA TIMU AGUNA...