Home news MIEZI MIWILI SASA TOKA ASAJILIWE..KIWANGO CHA BANDA CHAWASHTUA SIMBA..WACHUKUA HATUA HIZI

MIEZI MIWILI SASA TOKA ASAJILIWE..KIWANGO CHA BANDA CHAWASHTUA SIMBA..WACHUKUA HATUA HIZI


UONGOZI wa benchi la ufundi la Simba umeshtushwa na kiwango cha nyota mpya wa timu hiyo, Peter Banda, aliyesajiliwa kutokea klabu ya Nyasa Big Bullets ya Malawi.

Banda anayetajwa kuwa mrithi wa kiungo wa Msumbiji aliyejiunga na Al Ahly ya Misri, Luis Miquissone alitangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Simba Agosti 3, mwaka huu akitokea Nyasa Big Bullets.

Kabla ya kujiunga na Simba nyota huyo msimu uliopita wa 2020/21 alikuwa akiichezea timu ya FC Sheriff Tiraspol ya Moldova kwa mkopo akitokea Big Bullet, ambapo benchi la ufundi la Simba limekiri kuwa nyota huyo anakosa utimamu wa mwili na amepewa programu maalum.

Tangu ajiunge na Simba nyota huyo amecheza mchezo mmoja pekee wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United, huku pia akikosekana katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy uliochezwa Jumapili iliyopita.

Simba sasa inajipanga na mchezo wa marudiano dhidi ya Waswana hao utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salam Oktoba 24. Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha wa Viungo wa Simba, Adel Zrane alisema:

β€œBanda ni miongoni mwa wachezajibora sana ambao tumewasajili katika dirisha la usajili lililopita, na hasa katika mashindano ya kimataifa kwa kuwa amecheza soka katika michuano mikubwa Ulaya, lakini wakati anakuja alikuwa ametoka katika kipindi ambacho alikaa muda mrefu bila kucheza.

β€œHali hii ilisababisha akose utimamu wa mwili jambo ambalo lilitushtua, na kama benchi la ufundi kulazimika

kumpa programu maalum ya mazoezi anayoendelea nayo kwa sasa ili kuhakikisha anakuwa katika kiwango cha ushindani sawa na ugumu wa ligi yetu.”

SOMA NA HII  HUYU HAPA MTZ ALIYETOBOA BILA SIMBA NA YANGA ...KUTOKA KUCHEZA CHANDIMU MPAKA KUSAJILIWA NNJE YA NCHI..