Home Habari za michezo SIMBA TUMBO JOTO MECHI YAO DHIDI YA MTIBWA SUGAR…. ISHU IKO HIVI

SIMBA TUMBO JOTO MECHI YAO DHIDI YA MTIBWA SUGAR…. ISHU IKO HIVI

Habari za Simba SC

Licha ya kutopoteza dhidi ya Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu kwa miaka 10, beki wa Simba, Israel Mwenda anaamini mechi ya leo baina yao kwenye Uwanja wa Manungu Complex haitokuwa nyepesi kwa upande wao.

Mara ya mwisho kwa Mtibwa Sugar kupata ushindi dhidi ya Simba ilikuwa ni Februari 24, 2013 ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 na baada ya hapo haijapata ushindi katika mechi 20 mfululizo.

Katika mechi hizo 20 zilizopita baina yao, Simba imepata ushindi mara 13 na zimetoka sare mara saba, huku Simba ikifunga mabao 35 na Mtibwa Sugar ikipata mabao sita tu.

ALSO READ
Kitayosce yaanza Ligi kwa aibu
Soka 22 hours ago
Kisa penalti, Jonesia apewa shavu
Soka 22 hours ago
Mwenda alisema wanaamini Mtibwa Sugar itawapa mechi ngumu kesho hivyo wamejiandaa kisaikolojia kukabiliana nao.

“Mechi itakuwa ngumu kwani Mtibwa ni timu nzuri. Mechi zinatofautiana na timu haiwezi ikacheza vilevile kila siku. Jambo la muhimu tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti.

“Sisi tumejiandaa vizuri na naamini kwa sapoti ya mashabiki wetu, tutajituma kuhakikisha tunapata ushindi na kuwapa furaha,” alisema Mwenda

SOMA NA HII  KIZAAZAA CHA MZAMIRU YASIN KWENYE DABI, ROBERTINHO ALISEMA HIVI