Home Habari za michezo KIZAAZAA CHA MZAMIRU YASIN KWENYE DABI, ROBERTINHO ALISEMA HIVI

KIZAAZAA CHA MZAMIRU YASIN KWENYE DABI, ROBERTINHO ALISEMA HIVI

Habari za Simba sc

Mzamiru Yassin mwamba kabisa hana bahati na mechi kubwa, anaweza kupiga kazi kubwa dakika zote ila kosa lake moja likatumiwa na wapinzani kisha mashabiki wakaanza makelele.

Rejea mechi ya Simba 1-1 Yanga, bao la Aziz KI faulo nje kidogo ya 18 ikawapotezea poiƱti tatu wakakomba pointi moja.

Ngoma ilikuwa Oktoba 23 2022 muda mfupi kabla ya wapinzani hao kuelekea mapumziko Mzamiru alimchezea faulo Khalid Aucho kwenye harakati za kuokoa hatari.

Rejea mechi ya AFL dhidi ya Al Ahly bao la Kwanza Uwanja wa Mkapa mpira aliopoteza ngoma ilikwenda kuwa chuma.Mpira ni mchezo wa makosa hivyo mashabiki lazima ile presha isiwe kubwa.

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amesema kuwa makosa yaliyotokea kwenye mechi zilizopita wamefanyia kazi.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ACHAFUKWA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU SIMBA MBOVU